Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, leo amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora Region.
Katika ziara hiyo, Kihongosi ametembelea Shule ya Sekondari ya Bweni Puge iliyopo Kata ya Ndala ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni mawili, madarasa manne pamoja na ujenzi wa matundu kumi ya vyoo. Ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo huku akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa wakati ili kuwawezesha wanafunzi kupata mazingira bora, salama na rafiki ya kujifunzia.
Aidha, Kihongosi ametembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ambapo amejionea shughuli za utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Akiwa hospitalini hapo, amepongeza uongozi wa hospitali pamoja na uongozi wa wilaya kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na juhudi zinazoendelea za kuboresha huduma za afya, hatua ambayo imesaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa Wilaya ya Nzega.
Katika hatua nyingine, Katibu huyo wa NEC amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,DKT. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo muhimu ya maendeleo inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi.
Ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu wa Chama na Serikali wa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika na kuleta tija kwa wananchi.
MATUKIO KATIKA PICHA













Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa