Idara ya Maji katika Halmashauri ni idara inayosimamia utoaji wa huduma ya Maji vijijini ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa sera na sheria zote zinazohusiana na Maji kwa ujumla. Utekelezaji wa miradi ya Maji hufanyika kutokana na mpango na bajeti iliyopitishwa kwa mwaka husika. Pia matengenezo madogo madogo kwa miradi iliyopo hufanyika kulingana na maombi au taarifa zinazowasilishwa kutoka maeneo husika pindi miradi hiyo inapoharibika.
TAKWIMU ZA MIRADI YA MAJI ILIYOPO VIJIJINI
1.Miradi ya Maji ya bomba ni 14, Inayofanya kazi ni 10 isiyofanya kazi ni 4
MALENGO YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
1.Kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya maji.
2.Kufanya matengenezo ya vifaa vya ofisi na kugharamia mahitaji mbalimbali ya ofisi.
3.Kutoa mafunzo kwa watumiaji maji juu ya uendeshaji wa Miradi ya maji.
4.Kuwajengea uelewa jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira yanayowazunguka na kuwa navyoo bora kwenye kaya zao.
5.Kugharamia shughuli za ushauri (Consultancy) kwa miradi yamaji.
6.Ujenzi wa miradi 2 ya maji katika vijiji vya Upungu na Sigili.
7.Kufanya matengenezo ya magari 2 na pikipiki 2 za Idara ya maji.
MIRADI INAYOTEKELEZWA
1.MIRADI YA TEKELEZA SASA KWA MATOKEO MAKUBWA (BRN)
Miradi ya Maji inayotekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kupitia Idara ya Maji vijijini hadi sasa ni Miradi ya maji ya bomba katika vijiji vya Ngukumo, Mwambaha, Bukene na Sojo.
2.MIRADI YA WAFADHILI
Serikali ya Japan kupitia shirika la maendeleo (JICA) kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji wanatekeleza miradi ya maji ya visima virefu 44 na mradi wa maji ya bomba 1 unaohudumia kijiji cha Isanga.
3.MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA.
Utekelezaji wa Mradi wa Ziwa Victoria unategemea kuvinufaisha jumla ya vijiji 28 vya Usagari, Isunha, Upungu, Busondo, Nkiniziwa, Ngukumo, Mwambaha, Mwanhala, Utwigu, Itilima, Kipugala, Iboja, Ilagaja, Isanga, Mwaluzwilo, Kabale, Kanolo, Nata, Kilabili, Mwabangu, Chamipulu, Mbagwa, Mwakashanhala, Magengati, Inagana, Uhemeli, Iyombo na Kampala.
kazi zilizofanyika katika ngazi ya Halmashauri ni pamoja na kubainisha njia ya bomba kwenye vijiji vinavyopitiwa na mradi, kubaini na kuhaminisha nyumba na mashamba yatakayoathiriwa na mradi. Pia kazi ya uhamasishaji kupitia mikutano na wadau kuhusu kuachia mashamba kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya maji bila fidia.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa