• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe kwa Watumishi |
Nzega District Council
Nzega District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • sheria
      • Nyuki
      • TEHAMA
  • Fulsa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Vivutio katika Kilimo
    • Vivutio vya Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Utamaduni na Michezo
    • Maji
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Mipango na Utawala
      • kamati ya uchumi kazi na mazingira
      • kamati ya Elimu afya na maji
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Madili
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video za shughuli za ofisi
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
      • Elimu Msingi Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi
      • Sekondari Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • Kuweka Rangi
      • Afya Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi

HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAANZA UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KAYA WANUFAIKA WA TASAF

Posted on: February 11th, 2026

Nzega, Tabora

Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imeanza rasmi utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwa kaya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya kwa uhakika.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa zoezi hilo, Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Bi. Jovita Patrick, amesema jumla ya kaya 2,621 zenye wanufaika 10,614 kutoka kata mbalimbali za wilaya hiyo zitanufaika na mpango huo. Amesema lengo kuu la mpango huo ni kuwezesha kaya zenye uhitaji kupata huduma za matibabu bila vikwazo vya kifedha.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Ofisi Ndogo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Wilaya ya Nzega, Bw. Haji Mpeta, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa ngazi za kata na vijiji katika utambuzi na uthibitishaji wa kaya husika ili kuhakikisha walengwa wote wanafikiwa kwa wakati. Ameeleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Naye Diwani wa Kata ya Utwigu, Mhe. Christina Ikaji, amepongeza kuanza kwa zoezi hilo katika kata yake na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la uandikishaji na upokeaji wa kadi za bima ya afya. Aidha, ametoa shukrani kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuimarisha sekta ya afya nchini.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wameishukuru Serikali kwa kuwajali na kuwapatia fursa ya kupata huduma za afya kupitia mpango huo, wakieleza kuwa hatua hiyo itapunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa familia zao.

Zoezi la usajili na ugawaji wa kadi limefanyika katika vijiji vya Mwambaha, Isalalo, Utwigu, Mwanhala na Iyombo, na linatarajiwa kuendelea kwa siku 10 katika kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ili kuhakikisha walengwa wote wanapatiwa huduma hiyo muhimu.

MATUKIO KATIKA PICHA


Matangazo

  • MATOKEO YA PSLE 2025/DARASA LA SABA-MKOA WA TABORA November 05, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA WAKUSANYA MAPATO (REVENUE COLLECTORS) January 26, 2026
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE USAILI JIMBO LA BUKENE NA NZEGA VIJIJINI October 11, 2025
  • TANGAZO-WAMILIKI WA MAGARI September 30, 2025
  • Angalia yote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAANZA UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KAYA WANUFAIKA WA TASAF

    February 11, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAPOKEA POWERTILLER (TREKTA TEMBEZI) KUTOKA WIZARA YA KILIMO KUPITIA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

    February 03, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAFANYA KIKAO MAALUMU CHA KUJADILI MASUALA YA KIUTENDAJI NA MAENDELEO

    January 29, 2026
  • MKUU WA WILAYA YA NZEGA AADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA RAIS SAMIA KWA VITENDO: ATEMBELEA SHULE, ATOA ZAWADI, ATOA ONYO KALI KWA WANAOKIUKA HAKI YA ELIMU NA KUONGOZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI

    January 27, 2026
  • Angalia yote

Video

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAENDELEA KWA KASI
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Matukio
  • Habari Mpya
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa Zinazofanana

  • TAMISEMI
  • KARIBUNI NZEGA YETU
  • twitter
  • Instagram
  • Mkoa wa Tabora
  • Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana na sisi

    Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )

    Anuani ya Posta: S.L.P 4

    Telephone: 026 2692349

    Simu ya Kiganjani: 0765600994

    Barua pepe: md@nzegadc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa