• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe kwa Watumishi |
Nzega District Council
Nzega District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • sheria
      • Nyuki
      • TEHAMA
  • Fulsa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Vivutio katika Kilimo
    • Vivutio vya Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Utamaduni na Michezo
    • Maji
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Mipango na Utawala
      • kamati ya uchumi kazi na mazingira
      • kamati ya Elimu afya na maji
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Madili
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video za shughuli za ofisi
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
      • Elimu Msingi Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi
      • Sekondari Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • Kuweka Rangi
      • Afya Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi

HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAPOKEA POWERTILLER (TREKTA TEMBEZI) KUTOKA WIZARA YA KILIMO KUPITIA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

Posted on: February 3rd, 2026

Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imepokea zana za kisasa za kilimo aina ya powertiller (trekta tembezi) kutoka Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

Powertiller hizo zimegawiwa katika skimu za umwagiliaji zilizopo kwenye kata sita za Wilaya ya Nzega ambazo ni Sigili, Nata, Kamanhalanga, Budushi, Lusu na Ikindwa. Ugawaji huo unalenga kuwawezesha wakulima kutumia teknolojia ya kisasa katika shughuli za kilimo, kuongeza tija, kupunguza gharama za uzalishaji na kuondoa utegemezi wa zana duni za kilimo.

Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa zana hizo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Kilimo, kwa kuendelea kuwasogezea wakulima zana muhimu za uzalishaji. Aidha, amewahimiza wanufaika wa powertiller hizo kuzitunza ipasavyo na kuhakikisha zinawanufaisha wakulima wengi zaidi katika maeneo ya skimu za umwagiliaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Sehemu ya Kilimo Mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Said Shemahonge, amewataka wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya powertiller hizo kwa kufuata miongozo ya kitaalamu, ikiwemo kuepuka kuzitumia kubeba mizigo inayozidi uwezo wake, ili ziweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa muda mrefu.

Naye mmoja wa wakulima walionufaika na mpango huo ameishukuru Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, akieleza kuwa upatikanaji wa powertiller hizo utachochea ongezeko la uzalishaji wa mazao na kuboresha maisha ya wakulima.

Ugawaji wa powertiller hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, kuongeza uzalishaji wa mazao, kuhakikisha usalama wa chakula na kuinua kipato cha wakulima nchini.


Matangazo

  • MATOKEO YA PSLE 2025/DARASA LA SABA-MKOA WA TABORA November 05, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA WAKUSANYA MAPATO (REVENUE COLLECTORS) January 26, 2026
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE USAILI JIMBO LA BUKENE NA NZEGA VIJIJINI October 11, 2025
  • TANGAZO-WAMILIKI WA MAGARI September 30, 2025
  • Angalia yote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAPOKEA POWERTILLER (TREKTA TEMBEZI) KUTOKA WIZARA YA KILIMO KUPITIA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

    February 03, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAFANYA KIKAO MAALUMU CHA KUJADILI MASUALA YA KIUTENDAJI NA MAENDELEO

    January 29, 2026
  • MKUU WA WILAYA YA NZEGA AADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA RAIS SAMIA KWA VITENDO: ATEMBELEA SHULE, ATOA ZAWADI, ATOA ONYO KALI KWA WANAOKIUKA HAKI YA ELIMU NA KUONGOZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI

    January 27, 2026
  • WAHESHIMIWA MADIWANI NZEGA WAHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI KWA KUSISITIZWA TEHAMA NA MAADILI

    January 21, 2026
  • Angalia yote

Video

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAENDELEA KWA KASI
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Matukio
  • Habari Mpya
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa Zinazofanana

  • TAMISEMI
  • KARIBUNI NZEGA YETU
  • twitter
  • Instagram
  • Mkoa wa Tabora
  • Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana na sisi

    Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )

    Anuani ya Posta: S.L.P 4

    Telephone: 026 2692349

    Simu ya Kiganjani: 0765600994

    Barua pepe: md@nzegadc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa