NAWAAGIZENI HALMASHAURI ZOTE NCHINI HAKIKISHENI “MATERIALS” YOTE YANANUNULIWA TOKA VIWANDA VYA NDANI
Posted on: October 23rd, 2018
Mhe. Seleman Jafo Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aagiza halmashauri zote na taasisi zote nchini kutumia viwanda vya ndani kununua vifaa muhimu vya ujenzi kama , Mabati,Nondo Saruji na Vigae vya ndani. Aliyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la uzazi la kinamama katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega leo tarehe 23/10/2018 .
‘’Wakati mwingine mtu ukimwamini sana mwisho wa siku watu wanaharibu ndilo tatizo letu’’ aliyasema hayo alipokuwa katika kuongea na kamati ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Nzega. Mhe. Selemani Jafo aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakuwa na thamani ya Pesa, akisema kuwa ni vema pesa yote itakayobaki mara baada ya ujenzi wa wadi ya mama na watoto ya kisasa ioneshe “value for money” katika kila jingo litakalokarabatiwa. Pesa hiyo hapo awali ilikuwa itumike kwa maandalizi ya ujenzi wa hospital ya Wilaya katika maeneo ya karitu.
Aidha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega ndugu Sekiete S Yahaya alimweleza Waziri kuwa watahakikisha wanasimamia ujenzi huo kwa umakini na kuwa fedha itakayobaki mara baada ya kujenga wadi ya uzazi itakarabati wadi kubwa ya Bima ya Afya, wadi ya wazazi, X-Ray na wadi ya Watoto.
Mhe. Seleman Jafo alisifia shughuli zote zinazofanyika katika Halmashauri za wilaya ya Nzega(Mji na Wilaya), lakini aliwataadharisha kuwa wasibweteke kwa kazi hizo zilizoonekana Busondo,Unambewa, Lusu,Mwangoye na Zogolo. Tunataka tujenge kitu kizuri zaidi na nitakapokuja hapa tena nikute kitu cha tofauti,’ Mhe. Waziri alisema. Lakini pia aliridhishwa na aina ya tofali zinazotumika katika ujenzi wa majengo hayo kwani inaonekana sehemu nyingine tofali zimekuwa zikileta nyufa mara baada ya Ujenzi kukamilika .
Pia Mhe. Waziri alifurahishwa na kitendo cha ununuzi wa vifaa kutoka katika viwanda vya ndani. Alielekeza kuwa ununuzi wote wa Sementi, Mabati na Nondo ufanywe toka viwanda vyetu vya ndani kwani kuna viwanda vingine kama kilichopo Mkuranga na Kibaha Magodauni yamejaa nondo lakini wengine bado wananunua Nondo toka nje ya nchi. Fedha bilioni 33 zimesahaanza kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa Halmashauri hivyo basi alizitaka halmashauri zote nchini kununua bidhaa hiyo kwenye viwanda hivyo. Wizara yake inasimamia miundombinu mingi hivyo hatakubali kuona viwanda vya ndani vinakufa.
Aliwataka wakurugenzi kuongeza mwendo katika ujenzi na ukarabati kwani bado wako nyuma sana. Mhe.Waziri aliwashukuru kwa kumsikiliza na kasha alichukua picha za pamoja na watumishi na kasha aliendelea na safari yake kuelekea Dodoma.