KAMATI YA FEDHA MIPANGO NA UTAWALA YAMPONGEZA MKURUGENZI KWA USIMAMIZI WA MIRADI
Ikiwa ni katika kutekeleza majukumu ya kamati ya fedha Utawala na Mipango imekuwa msatari wa mbele katika kuhakikisha miradi iliyopo
Katika halmashauri ya Wilaya ya Nzega inatekelezwa kwa Ufani wa hali ya juu kwani wamekuwa na kawaida ya ufuatiliaji kila mwezi
na kila robo ya mwaka kwani ziara hizo zimekuwa na tija hasa katika uboreshaji wa utendaji katika ngazi ya kata.
Wajumb wa kamati hiyo baada ya kupitia miradi mbalimbali inayotekezwa kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024
walimpongeza mkurugenzi mtendaji Eng.modest Aplinary kwa namana mabyo ameweza kutengeneza mfumo mzuri wa usimamizi wa miradi
inayotekelezwa kwani thamani ya fedha inaonekana dhahili kutokana na ubora wa majengo yanayojengwa.
walisema kwa miradi ambyo wametembelea yenye thamani ya zaidi ya milioni 863 kila mradi unaonekana kuwa bora na unatekelezwa
kwa ufanisi hivyo wajumbe wakamuomba mkurugenzi kuendelea hasa kuwaongezea nguvu wahindisi amboa wamekuwa wakikihakikisha
miradi hiyo inajegwa kwa ufanisi.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa