Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya nzega ameongoza zoezi la kupanda miti zaidi ya 1000 katika maeneo yake ya utawala ikiwa ni katika eneo la barabara kuu iendayo Tabora mpaka Ndala na kisha kufanya bonanza lilifanyika katika Shule ya Sekondari Kampala,zoezi hilo limefanyika siku ya Jumamosi tarehe 04.01.2020.
Akiongea katika sherehe ya kukaribisha Mwaka 2020 ziliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya uliopo Nzega amewataka watumishi kuchapa kazi lakini pia kufanya maandalizi ya familia zao wangali bado na nguvu. pamoja na kufanya kazi Ndala mkurugenzi amesisitiza kuwa bado aseti zilizopo Nzega ni za halmashauri ya wilaya na tunaweza kuzitumia kwa namna yeyote.
Aliwataka watumishi kupiga hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kumtaka afisa utumishi kuanzisha saccos kwani zina msaada mkubwa kwa watumishi,alitoa mfano kwa shule ya mojawapo Ndala ifugayo samaki jinsi ilivyofanikiwa katika ufugaji wa Samaki hasa katika zoezi la ujazaji maji katika kisima cha kufugia ambalo huchukua muda mfupi kwa kuwatumia wanafunzi, alisema tujifunze kupitia umoja huo na zoezi hilo la ujazaji maji kwa muda mfupi ili tuwe na sccos yetu, aliendelea kuwa watumishi wengi hunyanyasika sana kwenye kukopa saccos ikiwa ni pamoja na kufirisiwa. tukiwa na saccos italeta umoja .
Aidha aliwataka watumishi kupendana kwani haitatokea mtu mwingine kuja kuwapenda wao, pendaneni, mtu akipata tatizo lichukue na kulifanya lako, ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri.
Mkurugenzi alisisitiza kufanya mazoezi kwa watumishi kwani asilimia kuwa ya watumishi hawafanyi mazoezi, ili kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari, watumishi hawana budi kufanya mazoezi. Tafiti zinaonesha kuwa watumishi wengi wanapatikana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa sababu ya kuwa na muda mwingi ofisini ,kazi zisije tuua hivyo anawataka afisa michezo na mganga mkuu kuweka program za mwaka huu kuhakikisha kuwa tunakuwa na mazoezi.
Mkurugenzi aliwasisitiza watumishi kutoogopa kufika ofisini kwake kwa lolote iwe ni mtu mmoja ama kikundi. aliwakaribisha kutoa changamoto zao ofisini mwake.