Akiongea katika siku ya tatu ya kufunga kongamano la fursa za uwekezaji wa Mkoa wa Tabora katika ukumbi wa Mwanaiyungi Mkuu wa Mkoa alisema kuwa yeye ni Mkuu wa Mkoa wa Wilaya nane ambazo wamekubaliana kuwa kila halmashauri itatekeleza majukumu waliyopewa . Halmashauri ya wilaya ya Nzega itawekeza katika fursa za Ranchi , wanyama na Mazao.
akieleza majukumu hayo Mkuu huyo alieleza kuwa Sikonge itawekeza katika Asali, Igunga itawekeza katika Mpunga,Nzega TC watawekeza katika kiwanda cha kuchakata Nyama, Uyui watawekeza katika Alizeti,Mansipaa watawekeza katika kiwanda cha utengenezaji nguo aina ya Jeans, Urambo watawekeza katika kiwanda cha Tumbaku na Kaliua watawekeza katika Ranchi na Misitu.
Akifunga kongamano hilo aliwaomba wadau dunia nzima kuja kuwekeza katika Mkoa wa Tabora palipjaa fursa za kutosha
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa