UTORO MASHULENI UDHIBITIWE
Mku wa mkoa wa tabora mhe. Agrey Mwanri amewataka watumishi kuhakikisha watokakomeza utoro mashuleni.
Hayo ameyasema leo 04 Aprili,2018 alipokuwa akifanya ziara wilayani Nzega. Ziara hiyo ililenga ufuatiliaji wa miradi inayofadhiliwa na Equip.
Aliyazungumza hayo akiwa katika Ukumbi wa Lake Tanganyika ambapo wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Nzega na Mji walikuwepo ikiwa ni Maafisa Elimu Kata na Watendaji wa Kata.
Aliserma Kulingana na Sera ya Elimu ya mwaka 2014 , wataalamu hao wanapaswa kuhakikisha wanafunzi wote waliandikishwa shule wanakuweopo mashuleni wakati wa mihula ya masomo.
Ameagiza ufuatiliaji wa karibu ufanyike mashuleni kwa kutumia daftari la Mahudhurio na kupitia vikao vya watumishi iwapo kutabainika kuna tatizo la utoro litatuliwe palepale.
Aidha amesema Mkoa wa Tabora ni Mkoa wenye heshima tangu enzi za ukoloni hivyo kama heshima yake imeshuka watapambana kuirudisha heshima hiyo.
Vilevile amewaagiza walimu kuhuisha taaarifa za wanafunzi mara kwa mara, na watoto watakaoonekana watoro kwa muda wa miezi mitatu 3 wafutwe kama sheria inavyotaka.
Amewataka kuchukua hatua kwa wanaofunga ndoa za utotoni na pamoja na kuwapa mimba wanafunzi na kuwanyima nafasi ya kuendelea na masomo.
Wote watakaobainika kufunga ndoa na watoto wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa