|
w |
W
|
aziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe. Januari makamba aliagiza kuwa kila kijiji kiunde kamati za mazingira,jinsia ikizingatiwa. Aliyasema hayo alipokuwa akitembelea kijiji cha Mwambaha na Ngukumo kujionea hali halisi ya maeneo ya hifadhi ya misitu iliyopo katika vijiji hivyo hivi karibuni.
Aidha Mhe. Waziri aliagiza kuwa shule zote za sekondari na msingi ziunde club za mazingira, pia aliagiza kuwa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata kuwepo na Afisa Mazingira.
Hata hivyo alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri akishirikiana na NEMC- National Environment menegement Council,TFS Tanzania Forest Service kuhakikisha wanakutana na kuona njia sahihi ya kuwekeza katika misitu mwingine kwa mujibu wa sheria No 20 ya mwaka 2004 sheria ya mazingira huku serikali ikijaribu kutafuta njia ya kuuchukua msitu huo na kuuhifadhi kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo viwili. Mhe. Makamba aliseme “tusiwaogope kwa kusema kuwa ni wakali, kwenye Dunia hii hajazaliwa mwanaume mkali kuliko Serikali ,serikali ndiyo yenye mabavu yote” aliongeza kuwa jiji la Dar-es-salaam linatumia asilimia 60 ya mkaa wote unaochomwa hapa nchini na jiji lenye kuwa na umeme na gesi kwa kwa matumizi ya nyumbani lakini wananchi wa Ngukumo wanabaki maskini na kutofaidika nao.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Makamba aliwataka wananchi wa vijiji vya Nkukumo na Mwambaha kuhakikisha wanazuia ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa ambao leo umesababisha maeneo mengi ya Wilaya ya Nzega kuwa jangwa,kukosa mvua za uhakika na maji kwa ajili ya mifugo yao.
Mheshimiwa Januari Makamba Mbunge wa jimbo la Bumbuli Lushoto Tanga alichangia kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati ya Mwambaha na vyoo vya Matundu 3 katika shule ya msingi Mwambaha.
|
MHE. Waziri alipanda miti miwili katika kijiji cha mwambaha na shule ya Msingi Mwambaha. Kijiji cha mwambaha kina hekta 23 na kijiji cha Ngukumo kina hekta 18 za msitu wa Hifadhi.
Mheshimiwa Waziri alikamilisha ziara yake mchana na kisha kuendelea na ziara yake mkoani Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa