• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe kwa Watumishi |
Nzega District Council
Nzega District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • sheria
      • Nyuki
      • TEHAMA
  • Fulsa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Vivutio katika Kilimo
    • Vivutio vya Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Utamaduni na Michezo
    • Maji
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Mipango na Utawala
      • kamati ya uchumi kazi na mazingira
      • kamati ya Elimu afya na maji
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Madili
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video za shughuli za ofisi
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
      • Elimu Msingi Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi
      • Sekondari Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • Kuweka Rangi
      • Afya Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi

MRADI WA MAJI ULIOKATALIWA MAHENE WAPOKELEWA.

Posted on: October 1st, 2018


MRADI WA MAJI ULIOKATALIWA  MAHENE WAPOKELEWA.



W


ananchi wa Mahene  na Buhondo wamekubali na kupokea miradi wa maji iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 430,000,000 Katika vijiji hivyo viwili. Mradi huo uliokuwa na awamu mbili katika kuukamilisha ulipokelewa kwa shangwe na wananchi hao wa Mahene. ‘’Kwa sasa tutapumua na kupunguza kero ya kuamka usiku kwenda kuteka maji katika maeneo ya visima ‘’alisikika mwananchi mmoja akieleza.

Akizindua mradi huo wa maji katika nyakati tofauti tofauti  Mkuu wa wilaya Mhe. Godfrey Ngupula aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanaitunza  miradi hiyo na kuwa walinzi wa miundo mbinu  hiyo ili kuweza kupunguza adha ya ukosefu wa maji katika vijiji hivyo ambayo imedumu kwa takribani  miaka minane sasa.

Katika kijiji cha Mahene Mkandarasi wa mradi huo Tingwa Company alipewa muda wa miezi tisa kuwa amekamilisha ukarabati wa miundombinu ya mradi huo.


M


kuu wa wilaya ya Nzega Mhe. Godfrey Ngupula,  kamati ya ulinzi na usalama  na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega ameendelea na ziara yake ya nne katika kusikiliza kero za wananchi katika kijiji cha  Mambali,Mbutu na Mogwa.

Mambali ni kijiji kilicho umbali wa kilometa takribani 85 toka Nzega mjini. Hivyo ilimlazimu mkuu huyo wa wilaya  kufunga safari yake kuelekea eneo ambalo lipo kusini Magharibi mwa Nzega. Mwenyekiti wa kijiji cha mambali Damson Msoma katika ufunguzi wake wa kikao aliwataka wananchi wa mambali  kutumia busara na hekima katika kusema kero zao na kuachana na  habari za kuokota mitaani ama kwenye vigenge vya kahawa.

Kero katika kijiji cha Mambali ,Mogwa  na mbutu hazikutofautiana sana , kwani kero nyingi zilikuwa ni kukosekana kwa miundombinu ya barabara  kwamba wakati wa masika barabara nyingi hazipitiki. Katika kujibu swali hilo Eng. Mwita Joram meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Nzega  alieleza kuwa barabara kukarabatiwa na  idara yake hutegemea na uhitaji wa matumizi kwa wakati huo ikiwa ni pamoja na  wananchi kuchukua hatua za dhati kuchangia nguvu zao na kuonesha mwelekeo kwa kukaa vikao vya kijiji na kata ili kupata ubarikio. Sifa hizo ni pamoja na  barabara  hiyo iwe na uhitaji wa kutosha na matumizi yake yawe makubwa.  Haiwezekani kutengeneza barabara inayotoka kijiji na kijiji wakati kuna barabara zenye kuunganisha  kata na kata ama tarafa na wakati mwingine kata na wilaya.

 Sekta ya Afya  ndiyo  yenye kuwa na  kero nyingi toka kwa wananchi , upungufu wa watumishi  na dawa ni  kero iliyoletwa na Peter Mayunga Mwananchi wa Mambali. Katika kujibu swali hilo  mwakilishi wa DMO Mganga mkuu wa Wilaya Ndugu Fraviunus Mark alisema kuwa  Mambali na Mbutu wamepewa  watumishi. Kwa upande wa dawa aliwataka wananchi kuhamasika vya kutosha ili kila kituo kipate pesa za kutosha  katika mfuko wa RBF, kwani  mama mjamzito akijifungulia  Zahanati ,  zahanati itachangiwa shilingi Elfu 25, lakini mama akihudhuria kliniki majuma mawili kabla atapata shilingi elfu 18 itakayoingia katika mfuko huo. Aidha kila msindikizaji atasaidia kuingiza kiasi cha  shilingi Elfu 8 kwa kila msindikizaji. Hii itasaidia kuwa na fedha za kutosha na hatimaye kufanya ununzi wa dawa katika zahanati  zetu.

Kutokumalizika kwa majengo limekuwa ni tatizo kubwa katika halmashauri ya wilaya ya Nzega. Hii yote imetokana na kuwa  na bajeti  kubwa na isiyofikiwa katika ukusanyaji. Mwaka 2017/18 makusanyo ya Halmashauri hayakuzidi asilimia 60%, ambayo ni hatari katika uendeshaji wa shughuli za maendeleo katika  Halmashuri ya Wilaya yetu. Kwa kutambua hilo Mkuu wa Wilaya ya Nzega   Godfrey  Ngupula  alisema kuwa  pamoja na kutengwa fedha Milioni 115 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Zahanati katika kijiji cha Mbutu itategemea na Makusanyo ya Ndani katika mwaka wa Fedha 2018/19. Aidha makadirio yameshafanywa na Eng. Wa  Ujenzi ili kupata gharama zitakazotumika katika kukarabati nyumba ya watumishi wa Zahanati.  Shule za Sekondari na Msingi zimekabiliwa na tatizo kama hilo karibuni vijiji vyote yaani kutokamilika kwa majengo.

Kutokana na wakulima wengi kutorudisha deni wanalodaiwa la pembejeo msimu uliopita  imeonekana kuwa ngumu kwao kukopeshwa pembejeo tena. Hivyo basi mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi kuhakikisha wanakusanya masalia ya mazao yote  na kuyachoma moto ili kuua wadudu wote waliokuwa wamesalia  shambani.

Wazee wengi hawana vitambulisho vya kutibiwa bure. Mkuu wa Wilaya Mhe. Godfrey Ngupula  anamuagiza mkurugenzi  kuhakikisha kuwa kufikia tarehe 30/10/2018 vitambulisho hivyo viewe vimekamilika.

Wananchi John Nicholous mkaazi wa Mogwa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya shule alilalamika kuwa agizo kutoka juu lilikuja kuwaeleza kuwa kwa mradi waliochagua wa kuku wataletewa kupitia mzabuni, kwa maelezo yake mwananchi huyo alisema kuwa lilikinzana na maamuzi yao ya awali kwamba watanunua vifaranga wa kuku wa kienyeji. Pamoja na agizo hilo ndugu John Nicholous akiwa mwenyekiti wa shule hiyo aliweka saini kuidhinisha matumizi ya fedha hiyo kwa mabadiliko hayo. Kutokana na kero hiyo alimwomba mkuu wa wilaya asaidie kujua huyo aliyeko juu ni nani?  Mhe. Godfrey Ngupula Mkuu wa Wilaya ya Nzega alitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kuwa anataka taarifa kamili ya mchakato mzima  wa zoezi hilo ulivyoendeshwa ndani ya siku 14. Alimtaka Mkurugenzi kuleta timu ya Mkaguzi wa Ndani kufika shuleni hapo ili kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo.

Ziara ya mkuu wa wilaya ilikomea katika kijiji hicho kwa siku hiyo akitaraji kuendelea na ratiba yake siku inayofuata katika kata ya Bukene.

Matangazo

  • MATOKEO YA PSLE 2020/DARASA LA SABA December 18, 2020
  • MAJINA YA MAKARANI WALIOITWA KWENYE USAILI JIMBO LA NZEGA VIJIJINI December 18, 2020
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI DARAJA LA III July 08, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI DARAJA LA III July 08, 2022
  • Angalia yote

Habari mpya

  • ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA

    October 08, 2024
  • KAMATI YA FEDHA UTAWALA NA MIPANGO YAMPONGEZA MKURUGENZI KWA USIMAMIZI WA MIRADI

    September 05, 2024
  • UBORESHAJI WA LISHE UWE NA MATOKEO CHANYA YA KIELEIMU

    February 07, 2024
  • UBORESHAJI WA LISHE UWE NA MATOKEO CHANYA YA KIELEIMU

    February 07, 2024
  • Angalia yote

Video

HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAHAMISHIA SHUGHULI ZA KIOFISI NDALA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Matukio
  • Habari Mpya
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa Zinazofanana

  • TAMISEMI
  • KARIBUNI NZEGA YETU
  • twitter
  • Instagram
  • Mkoa wa Tabora
  • Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana na sisi

    Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )

    Anuani ya Posta: S.L.P 4

    Telephone: 026 2692349

    Simu ya Kiganjani: 0765600994

    Barua pepe: md@nzegadc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa