Timu ya wataalamu wa ufuatiliaji na tathmini kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, mapema leo imefanya ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali za Mitaa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Mkoa katika kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo kila mwaka, kwa lengo la kukagua hali ya utekelezaji wa miradi na kujiridhisha na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali. Kwa mujibu wa mpango huo.
Miradi inayokaguliwa inahusisha sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu, Kilimo, Maji na Miundombinu ya Barabara. Katika Sekta ya Afya, timu imekagua miradi ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya vinavyojengwa kwa mpango wa TMCHP, zahanati, ujenzi wa vyoo, vichomea taka, pamoja na miundombinu ya Placenta Pit na Ash Pit.
Kwa upande wa Sekta ya Elimu, ukaguzi umefanyika kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa kupitia programu za GPE–TSP na SEQUIP, nyumba za walimu, mabweni, shule mpya za msingi na sekondari (SEQUIP) pamoja na utekelezaji wa mradi wa EP4R.
Timu ya ufuatiliaji imejumuisha wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwemo Ramadhan Mpolanje, Mchumi; Pelagia Tiliya, Muhasibu; na Alex Mhanga, Afisa Biashara, wakishirikiana kwa karibu na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Picha zinaonesha timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakiwa kwenye ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo





















Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa