Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Nzega na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kutumia mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayoendelea ili kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha utendaji bora wa Halmashauri katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akifungua mafunzo hayo leo tarehe 19 Januari, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la Ipazi, Mhe. Tukae amesisitiza umuhimu wa kila kiongozi kusimama katika nafasi yake na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria.
“Ninaomba kila mmoja asimame katika nafasi yake kwa sababu yale tutakayojifunza hapa naamini yatatusaidia kuibua vyanzo vipya vya mapato. Kila mmoja ataweza kufanya jambo jipya ndani ya kipindi hiki cha miaka mitano. Tusione miaka mitano kuwa ni mingi sana, bali tuitumie kama fursa ya kujifunza kuhusu utawala bora na misingi ya sheria ili tuweze kuibua vipaji na ubunifu katika utendaji wetu,” alisema Mhe. Tukai.
Mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea Madiwani uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya kisheria, usimamizi wa rasilimali na uongozi wenye tija, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 19 Januari hadi 21 Januari, 2026, na yatahitimishwa rasmi kwa kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa yale yote yatakayojifunzwa.
Madiwani wa Nzega wakishiriki mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kwa lengo la kuongeza ufanisi na ubunifu katika utendaji wa Halmashauri.










Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa