‘Kuna changamoto kubwa tumeiona Watoto wetu Nzega vijijini hawafanyi vizuri katika kumaliza elimu ya msingi” Waziri wan chi ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo alipokuwa akipokea taarifa toka kwa mkuu wa wilaya ya nzega jana ambayo katika ukumbi wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Zamani. Alisema kuwa ufaulu wa Watoto umeonekana kwamba kila Watoto 100 watoto 44 hawafaulu mitihani ,hivyo hili ni changamoto, kwani kitaifa kati ya Watoto 100 watoto 80 wanafaulu mitihani. Mhe. Ummy Mwalimu amesema kwamba uwiano wa walimu na wanafunzi sim baya ukilinganisha na maeneo mengine ambayo mwalimu mmoja huwa na wanafunzi 200 na kuendelea wakati Nzega mwalimu mmoja anafundisha Watoto 76 , uwiano huu si mbaya.
Mheshimiwa Waziri alipojaribu kutaka kujua tatizo n inini kinachofanya Watoto kutofaulu vizuri, Afisa Elimu Shule za Msingi ndugu Sistaimelida alijibu kuwa ni kutokana na mwamko duni wa elimu kwa wazazi na wakati mwingine huzuiwa na wazazi kwenda shule au kufanya mitihani.
Kwa changamoto hiyo Waziri aliagiza kwa mkuu wa Mkoa wa Tabora ahakikishe anachukua hatua kali kwa Watoto wote wafanyao utoro yeye,wazazi na walezi wake na wasiruhusu na kuwachekea wazazi wa Watoto watoro katika mkoa wa Tabora.
Aidha Waziri amehimiza uandikishaji wa Watoto wote awali na darasa la kwanza kwani mpaka sasa wameandikishwa Watoto 19/100. Wahimizeni watendaji na viongozi wote kuhakikisha wanafuatilia na kuhimiza uandikishaji kwenye maeneo yao. Pia Waziri ameimtaka Mkurugenzi kupitisha matangazo ili kuhimiza uandikishaji mashuleni.
Kwa shule za msingi Waziri ameona kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa hivyo serikali italifanyia kazi.
Amemtaka mkurugenzi kuhakikisha KUWA kusiwepo vikwazo kwa wanafunzimwote wanaoanza masomo yao ,wasizuiliwe kuanza masomo kwasababu ya ukosefu wa nguo za shule.wazazi hao wapewe muda kama majuma kadhaa ama mwezi na sikwa wanafunzi wote bali waanzao masomo.
Pia Waziri ameagiza kuwa tamisemi iangalie uwiano wa walimu wa masomo ya Sayansi kwa shule za Sayansi kama kuna changamoto basi tuweze kuwasaidia.
Akipokea maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt Batlida Buriani amemtaka mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha anapitisha matangazo kila sehemukuwataka Watoto wote ambao hawajajiandikisha wakafanye hivo, kufikia tarehe 31/12/ tutaanza msako, Hii ni aibu kwa mkuu wa mkoa mwenye PhD na Mbunge wa Jimbo Mwenye PhD kutofanya vizuri kwani hii ni aibu.
Pamoja na hayo yote Mhe. Waziri ameitaka Halmashauri kuongeza bidi z kusanyaji mapato kwani mpaka kufikia mwezi Novemba ukusanyaji umefikia asilimia 44%. Mko chini sana.
Kuhusu ujenzi wa Halmashauri Waziri amesema atatuma wataalamu wake wa uendelezaji mji wafanye topographiko survey ya jiombo lote la nzega vijiji ili yeye kama Waziri afanya maamuzi kama Waziri. Aidha atamshauri mwenye mamalaka afanye maamuzi kuipeleka mojawapo ya majimbo haya mawili kulipeleka mjini. Kufikia tarehe 30/02/2022 atakuwa ametoa majibu. Maamuzi hayo yatazingatia upatikanaji wa huduma kwa wananchi kwa urahizi.
Mheshimiwa Waziri alikagua mradi wa ujenzi wa madarasa matatu(3)shule ya Sekondari Kampala ambayo tayari ilikuwa imekamilika kwa kutumia kiasi cha Tsh Mil33.2 mpaka kukamilika. Alimpongeza Mkuu wa Shule kwa ukamilishaji wa mradi huo,aidha amemshukuru Afisa Elimu Kata ya Ndala kwa usimamizi mzuri wa ufaulu na uandikishaji.
Isidori Mayagilo
ICTO-NzegaDC
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa