Waziri waHabari na Michezo amesema kuwa Mkoa wa Tabora una kila kitu kufaa kuwekeza, aliyasema hayo leo katika kongamano alipokuwa akihitimisha kongamano la fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Tabora ukumbi wa Isike -Mwanakayungi ulipo Ofisi za Mkoa Tabora. Katika majumuisho hayo DKT. Halson Mwakembe alishukuru wajumbe wote katika kongamano hilo kwa ushiriki wao na kwa michango yao katika kongamano hilo. Aidha Waziri Mwakembe alimshukuru sana Joseph Simbakalia ambaye ni Mkurugenzi wa EPZA Mtaalamu wa Viwanda kwa elimu yake ya aliyoitoa jana ambayo ilijikita sana katika kujua dhan ya kujenga uchumi na Utayari wetu kama mkoa kuzingatia mambo matano ambayo ndiyo wawekezaji wanayahitaji. mambo hayo aliyataja kuwa ni :-
1. Ardhi na Barabara
2. Umeme wa uhakika
3. Wafanyakazi wenye stadi
4.Miundombinu ya usafirishaji
na Vivutio vya uwekezaji.
Mambo hayo kama tutayazingatia ni hakika tutapiga hatua kusonga mbele. ili kufikia hatua hizo Mhe. Waziri alisema ni vema kuachana na urasimu katika utaji wa viwanja na maeneo kwa wawekezaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa