Mkuu wa wilaya ya Nzega Adivera bulimba amsema kundi la uhalifu lililokuwa likijiita roho saba tayari limetokomezwa na vyombo vya dora na watuhumiwa wote watafikishwa mahakaman kujibu tuhuma zitakazo wakabili.
Adivera amesema kundi hilo la watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 15 lilianza kuvamia watu na kufanya uhalifu mbalimbali hali iliyosababisha kutishia amani ya wakazi wa Nzega.
Amesema vyombo vya dora vimefanya kazi kubwa ya kuwakamata vijana hao na muda wowote watafikishwa mahakamani.
Amesema wilaya ya Nzega iko salama na hakuna kundi wala kikundi kitakacho tishia amani ya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0765600994
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa