• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe kwa Watumishi |
Nzega District Council
Nzega District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • sheria
      • Nyuki
      • TEHAMA
  • Fulsa za Uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Vivutio katika Kilimo
    • Vivutio vya Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Utamaduni na Michezo
    • Maji
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Mipango na Utawala
      • kamati ya uchumi kazi na mazingira
      • kamati ya Elimu afya na maji
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Madili
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video za shughuli za ofisi
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
      • Elimu Msingi Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi
      • Sekondari Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • Kuweka Rangi
      • Afya Picha Kovid 19
        • Boma
        • kupaua
        • uwekaji wa rangi

MKUU WA WILAYA AKABIDHI FEDHA MILILIONI 47 KWA VIKUNDI 38

Monday 12th, May 2025
@Nzega

Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega Afisa Tawala  Charles S. Makwaya amepokea na kukabidhi kiasi cha shilingi Milioni arobaini na saba ikiwa ni pesa toka mapato ya ndani kwa vikundi 38. Vikundi 15 vya vijana na vikundi 23 vya kina mama, zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega leo.

Akizungumza na wanavikundi hao Afisa Tawala alisema kuwa mikopo hii ni ya lazima kwa mujibu wa sheria ya fedha ya mwaka 2018   kifungu namba 37A.  Alisisitiza kuwa mikopo hiyo haina riba kwa mujibu wa kifungu Namba 3, na huo ni upendo mkubwa toka Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa wananchi wake.

Aidha Afisa tawala huyo akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nzega alieleza aina tatu za uchumi wa kati kuwa ,  uchumi wa chini ni uchumi unaohangaikia fedha za kitanzania shilingi elfu kumi kwa mwaka, uchumi wa kati wa chini ni ule unaohangaikia kati ya shilingi milioni miambili hamsini hadi milioni mianane kwa mwaka na ule uchumi wa kati wa juu ni ule unaozidi milioni mianane kwa mwaka.

Aliwashukuru wanavikundi kwa kutumia fursa hii ya kutumia mikopo hii alisema kuwa fedha tayari zimeingia katika akaunti za vikundi 38. Akisoma risala kwa mgeni rasmi afisa maendeleo vijana  Jovitha Patrick alisema kuwa halmashauri ikiwa imekusanya bilioni 479 imeamua kutenga kiasi cha shilingi milioni 24 kwa ajili ya vijana  ambao ni vikundi 15 lakini shilingi milioni 25 itaenda kwa wanawake. Kutengwa kwa fedha hizo kunatokana na agizo la serikali kuwa kila halmashauri zinapaswa kutenga asilimia 10% ya mapato yao kwa ajili ya vijana na kina mama. Alisema katika zoezi hili walemavu hawajaingizwa bado lakini mgawanyo wao ni kama ifuatavyo:- vijana asilimia 4%, wanawake asilimia 4% na walemavu asilimia 2%, kwamba walemavu wataanza kutumia asilimia hiyo 2% katika mwaka ujao wa fedha.

Mhe.Kiwele Michael Bundala Diwani wa Mbutu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega alisisitiza matumizi mazuri ya Mikopo hiyo na kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kwa malengo na makusudio ya kikundi na wala si vinginevyo. Pamoja na matumizi hayo Mhe. Mwenyekiti alivitaka vikundi hivyo kuhakikisha vinakuwa na marejesho mazuri ili kutengeneza imani ya kuongeza mikopo hiyo na wakati mwingine kuvisaidia vikundi vingine kuweza kukopa.  Mhe. Kiwele Bundala aliutaka uongozi wa halmashauri kufuatilia kuona ni jinsi gani wanavikundi watasaidiwa kuepuka makato toka katika mabenki.

Mweka hazina wa halmashauri akichangia kabla ya mgeni rasmi kusimama alieleza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kwamba wahusika hutumia majina binafsi katika uwasilishaji wa pesa benki ambao hupelekea isijulikane hiyo fedha inatoka kwa kikundi gani, hivyo hupelekea na kuonesha kuwa hakuna vikundi ambavyo vimekwisha fanya marejesho, aliwataka wanavikundi kuhakikisha wanatumia majina ya kikundi husika  ili iwe rahisi kutambua, na mara baada ya malipo hayo hati ya malipo iletwe ofisi ya Fedha na si mtu kukaa nayo nyumbani.

Nipige tafu ni jina la kikundi linalomaanisha kuwa wanatamani kutoka hatua waliyokuwanayo, ambayo ni ya chini kwenda juu zaidi kwa kuongezewa nguvu na serikali ni kikundi kutoka Mbutu ambacho kilianza 2016 chini ya mwenyekiti Rahel Nyanza. Katibu wa kikundi hicho ndugu Emmanuel Maganga Kibela aliishukuru Serikali yake hasa Rais John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka Vijana wa kitanzania na hivyo aliwataka vijana wenzake wajiunge kwenye vikundi ili kujikwamua kiuchumi.  Kwa mujibu wa maelezo ya Katibu wa kikundi hicho alieleza kuwa kikundi chao kinajishughulisha na mambo makuu matatu ambayo ni uselemala,mamalishe na ushonaji wa nguo na kwa hakika watakuwa mabalozi wazuri wa kufanya marejesho.

Matangazo

  • MATOKEO YA PSLE 2020/DARASA LA SABA December 18, 2020
  • MAJINA YA MAKARANI WALIOITWA KWENYE USAILI JIMBO LA NZEGA VIJIJINI December 18, 2020
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI DARAJA LA III July 08, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI DARAJA LA III July 08, 2022
  • Angalia yote

Habari mpya

  • ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA

    October 08, 2024
  • KAMATI YA FEDHA UTAWALA NA MIPANGO YAMPONGEZA MKURUGENZI KWA USIMAMIZI WA MIRADI

    September 05, 2024
  • UBORESHAJI WA LISHE UWE NA MATOKEO CHANYA YA KIELEIMU

    February 07, 2024
  • UBORESHAJI WA LISHE UWE NA MATOKEO CHANYA YA KIELEIMU

    February 07, 2024
  • Angalia yote

Video

HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA YAHAMISHIA SHUGHULI ZA KIOFISI NDALA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Matukio
  • Habari Mpya
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa Zinazofanana

  • TAMISEMI
  • KARIBUNI NZEGA YETU
  • twitter
  • Instagram
  • Mkoa wa Tabora
  • Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana na sisi

    Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Kata ya Utwigu kijiji cha Mwambaha Lubisu )

    Anuani ya Posta: S.L.P 4

    Telephone: 026 2692349

    Simu ya Kiganjani: 0765600994

    Barua pepe: md@nzegadc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa