HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA
1: IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni moja kati ya idara 13 za Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ambayo ina jumla ya watumishi 6. kati yao Mtakwimu ni 1 na Afisa mipango (Wachumi) 5.
2:0 UTAWALA NA JIOGRAFIA
2:1 Utawala
Wilaya ya Nzega ina jumla ya Tarafa 4, Kata 36, Vijiji 158 na Vitongoji 964 na ikiwa na majimbo 2 ya uchaguzi, ambayo ni jimbo la Bukene na jimbo la Nzega Vijijini. Aidha Halmashauri ina jumla ya madiwani 51 kati yao madiwani 36 ni wa Kata na Madiwani 13 ni Viti Maalumu na Wabunge 2
2.2 Hali ya hewa
Wilaya ya Nzega hupata mvua kati ya 650mm na 1,200mm kwa mwaka. Msimu wa mvua huanza mwezi Novemba na kuishia mwezi April/May, kiwango cha juu cha joto ni 30oc na kiwango cha chini cha joto ni 28oc.
2:3 Idadi ya Watu
Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012, Wilaya ya Nzega ina wakazi wapatao 414,392 kati yao me ni 201,952 na ke ni 212,440 (Hii ni baada ya mgawanyo wa mji wa Nzega na Wilaya).
2:4 Hali halisi ya Wilaya katika Ajira, Kipato na Ustawi wa jamii
Katika mwaka 2015 pato la mtu katika Wilaya linakadiliwa kuwa Tshs. 420,000/= Kwa mwaka. Shughuri za kiuchumi za wakazi wa Nzega ni kilimo, ufugaji, biashara, ajira kutoka serikalini na ajira binafsi. Hata hivyo ustawi wa jamii katika Wilaya ya Nzega unategemea zaidi Kilimo na ufugaji.
3:0 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA IDARA KWA MWAKA 2016/2017
Idara ya mipango, takwimu na ufuatiliaji imejipanga kutekeleza majukumu yafuatayo;
4:0 MIRADI ILIYOPANGWA KUTEKELEZWA-2016/2017
Wilaya ya Nzega kupitia Mpango na Bajeti wa mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kutumia jumla ya Tshs. 1,767,888,868/= kutoka mapato ya ndani na kati ya hizo Tshs. 696,826,000/= ni matumizi ya kawaida na Tshs. 1,071,299,000/= ni miradi ya maendeleo.
Pia Wilaya ya Nzega imeidhinishiwa kupokea jumla ya Tshs. 10,144,317,000/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo Tshs. 2,254,169,000/= ni kutoka Seikali kuu na Tshs. 7,890,148,000/= kutoka kwa wafadhili. Aidha vipaumbele hasa vipo katika Ujenzi/ukamilishaji wa nyumba za walimu, madarasa, matundu ya vyoo, barabara, zahanati, uchimbaji wa visima vya maji na kutoa fursa za kujiajili kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu hasa kwa vijana na akina mama.
5:0 FURSA ZILIZOPO WILAYA YA NZEGA
Wilaya ya Nzega ina fursa nyingi zinazofaa kwa uwekezaji ikiwepo ardhi/eneo kubwa la uwekezaji kama vile;
5:1 Eneo Lililogunduliwa kuwa na Madini
Eneo la Uduka ambalo limegundulika kuwa na madini ya almasi na Malilita (Wela), hili eneo limegundulika kuwa na madini ya dhahabu, hivyo wawekezaji wanakaribishwa
5:2 Eneo linalofaa kwa Kilimo
5:3 Eneo linalofaa kwa ufugaji
hivyo wawekezaji makini wanakaribishwa.
5:4 Eneo la hifadhi
Eneo la hifadhi la pori kwa ajili ya uzalishaji wa asali lina ukubwa wa ha.118.798. wawekezaji wanakaribishwa kwa kuwekeza viwanda vya uzalishaji zao la asali
Pia Wilaya ya Nzega inazalisha kwa wingi mazao ya ngozi, mpunga, Tumbaku, Pamba na maembe hivyo wawekezaji wanahitajika kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya usindikaji wa mazao hayo. Aidha, Nzega ina fursa kama, hali nzuri ya hewa ikiwemo mvua za kati ya 650mm na 1,200mm kwa mwaka, rasilimali watu, Miundo mbinu endelevu hasa umeme na barabara zinazopitika, ukarimu wa watu wake na Sera nzuri za uwekezaji.
1:1 Dira – Kuwa na Halmashauri yenye uwezo wa kutoa huduma bora
na endelevu kwa Wadau wote
1:2 Mwelekeo – Kuwa na Halmashauri kutoa huduma endelevu za Kijamii na za Kiuchumi kwa kuwashirikisha Wadau wote.
1:3 Kaulimbiu – Ushirikishwaji wa Wananchi wote kwa maendeleo endelevu ya Wilaya ya Nzega.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa