Kitengo cha ukaguzi wa ndani kinatekeleza shughuli zake kwa lengo la Kutoahuduma za ushauri kwa Afisa Masuhuli juu ya utunzaji sahihi wa rasilimali zaHalmashauri. Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzegakimeanzishwa mwaka 2002na kwa sasa Kitengo kinawatumishi wawili (2) kwa maanaya Mkuu wa Kitengo na Msaidizi mmoja.
Miongoni mwa majukumu ya kitengo hiki ni kama ifuatavyo:-
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa ndani (Internal control),utunzaji na uangalizi wa matumizi ya rasilimali fedha zote za Halmashauri;
• Kupitia na kutoa ripoti juu ya kufuata taratibu za kifedha na kiuendeshaji kamazilivyoainishwa katika sheria, kanuni, au maelekezo yaudhibiti wa matumizi yaHalimashauri;
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya upangaji sahihi na mgawanyo wa mapato namatumizi ya Halmashauri;
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya matumizi sahihi ya fedha ili kuendana naviwango vya kimataifa;
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya uendeshaji au programu na kuhakikisha kuwamatokeo yake yanaendana na Malengo na madhumuni yaliyowekwa;
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya hoja za ufanisi wa kiutendaji wa menejimentikulingana na taarifa za mkaguzi wa ndani, na kuisaidia menejimenti katikautekelezaji wa mapendekezo yaliyoyopatikana kutokana na taarifa, na kufuatiliautekelezaji wamapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali;
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya ufanisi wa mifumo ya udhibiti yakielekitroniki iliyopo Halmashauri.
• Kuandaa na kutekeleza mpango kazi wa ukaguzi
• Kukagua taarifa za tathmini ya miradi ya maendeleo
• Kufanya uthaminishaji wa kiutendaji kwa ajili ya ukaguzi wa fedha n.k
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa