Kitengo cha Uchaguzi ni moja ya vitengo sita vya Halmashuri ya Wilaya ya Nzega. Kitengo hiki kinashughukia uratibu wa chaguzi mbalimbali na uanzishwaji wa maeneo mapya ya Utawala.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ina Majimbo mawili ya Uchaguzi, Jimbo la Bukene na Jimbo la Nzega Vijijini, Tarafa nne (4), Kata 36, Vijiji 158 na Vitongoji 965.
Katika Halmashauri kuna vyama kumi na tatu (13) vyenye Ofisi na uongozi. Vyama hivyo ni : ACT, AFP, CCM, CHADEMA, CUF, NCCR – MAGEUZI, NRA, TADEA, UMD, UDP, MAKINI, SAU na UPDP.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani, jumla ya vyama saba (7) viliweka wagombe kuwania nafasi mbali mbali za uongozi. Vyama hivyo ni : ACT, CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, SAU na TADEA.
Vituo 503 vilitumika kupigia kura. Kati yake, vituo 240 ni vya Jimbo la Nzega Vijijini na vituo 263 ni vya Jimbo la Bukene
Jumla ya wapiga kura 174,920 walijiandikisha kupiga kura katika Daftari la kudumu la wapiga kura. Waliojitokeza kupiga kura siku ya kupiga kura tarehe 25/10/2015 ni 93,634, sawa na 54% ya waliojiandikisha.
Urais:
Mhe. Magufuli, John Pombe alipata kura 69,319 sawa na 74% ya kura zote zilizopigwa.
Ubunge:
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa