IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ina wajibu wa kusimamia shughuli za kilimo na ushirika katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega. Idara hii inao watumishi 74 kati ya watumishi hao Maafisa kilimo ni 5, Maafisa kilimo wasaidizi ni 66, Mafundi Sanifu Umwagiliaji ni 2, Maafisa Ushirika ni 2.
1. Takwimu za msingi.
• Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ina jumla ya hekta 283,200 zinazofaa kwa kilimo.
• Eneo linalolimwa ni hekta 128,000
• Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 25,500
• Eneo linalomwagiliwa ni hekta 3,540
• Idadi ya kaya za wakulima ni 72915
• Idadi ya wakulima ni 130,592
• Idadi ya kaya zinazotumia wanyamakazi ni 28616
2. Malengo ya kilimo
Katika msimu wa kilimo wa 2016/2017 jumla ya hekta 195,482 ya mazao ya chakula, hekta 14,386 ya mazao ya biashara na hekta 595 ya mazao ya bustani zinatarajiwa kulimwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
3. Miradi ya maendeleo
Idara inatekeleza mradi wa Miundombinu ya masoko, uongezaji wa thamani katika mazao na huduma za kifedha vijijini (Market Infrastructure, value addition and Rural Finance Support (MIVARF) kipengele cha kunjengea uwezo mkulima na kumuunganisha na masoko (Producer Empowerment and Market Linkage (PEML). Mradi huu unatekelezwa na mtoa huduma BACLEMA CO.LTD katika vijiji vya Malolo Kata ya Ikindwa, Upambo kata Isanzu na Mwaguguli Kata ya Mwangoye. Halmashauri ipo kwenye mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya umwagiliaji wa Lusu na Kahamanhalanga.
4. Fursa zilizopo
Halmashauri ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumika ikiwa ni pamoja na hekta 25,500 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa