IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega katika kutekeleza majukumu yake inahitaji rasilimali watu ya kutosha ili kufikia malengo yake kwa ufanisi, Halmashauri kwa sasa inajumla ya watumishi 2,756 kati yao wanawake ni 1,117 na wanaume ni 1639. Ufuatao ni mchanganuo wa watumishi kwa kila idara/kitengo:-
MAJUKUMU YA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI
1. Kusimamia masuala ya ajira za watumishi wote wa Halmashauri |
2. Kusimamia uthibitishwaji wa watumishi kazini |
3. Kusimamia upandishwaji wa vyeo vya watumishi |
4. Kuandaa mpango kazi na kusimamia suala la mafunzo ya watumishi kazini |
5. Kusimamia shughuli za mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara |
6. Kusimamia nidhamu ya watumishi |
7. Kusimamia ufanyikaji wa vikao vya Kisheria vya Halmashauri na kikao cha idara ya Utawala na utumishi kwa kila mwezi |
8. Kuandaa na kusimamia ikama na bajeti ya mishahara ya watumishi
9. Kuandaa TANGE ya watumishi 10. Kuandaa taarifa za watumishi za robo mwaka 11. Kusimamia zoezi la upimwaji wa utendaji kazi kwa watumishi (OPRAS) |
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Mtaa wa Umbi)
Anuani ya Posta: S.L.P 4
Telephone: 026 2692349
Simu ya Kiganjani: 0784364828
Barua pepe: md@nzegadc.go.tz
Hati miliki Halmashauri ya Wilaya ya Nzega @ 2017. Haki zote zimehifadhiwa